48. Ni lazima kufanya ´Umrah katika Ramadhaan?

Swali 48: Baadhi ya watu wana imani kwamba kufanya ´Umrah katika Ramadhaan ni jambo la lazima kwa kila muislamu na kwamba ni lazima kufanya hivo angalau mara moja katika umri.

Jibu: Hili si kweli. Ni lazima kufanya ´Umrah mara moja katika umri. Haiwajibiki zaidi ya hivo. ´Umrah katika Ramadhaan imependekezwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“´Umrah katika Ramadhaan inalingana na kufanya hajj.”

Tunamuomba Allaah atuwafikishe sisi na ndugu zetu waislamu katika yale anayoyapenda na kuyaridhia. Kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kutoa, Mkarimu. Himdi zote ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 02/05/2021