48. Hakuna mtu mwenye akili anayefikiria hivo

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Daima alikuwa ni Mwenye sifa na majina Yake. Ametakasika kutokamana na kuwa sifa Zake ni zenye kuumbwa na majina Yake ni yenye kuzuka.

MAELEZO

Hakupata sifa yoyote baada ya kwamba hakuwa nayo hapo kabla. Majina na sifa Zake hazitengani Naye. Hazina mwanzo kama ambavo Yeye Mwenyewe hana mwanzo. Hazina mwisho kama ambavo Yeye Mweneywe hana mwisho. Allaah kwa majina na sifa Zake ndiye wa Kwanza, wa Mwisho, Mwenye kudhihiri na Aliyejificha. Hapa wanaraddiwa wale wanaokanusha majina na sifa za Allaah, kama vile Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah, na kusema kwamba majina na sifa za Allaah zinapelekea kumfanya Allaah kuwa na washirika. Ndio maana miongoni mwa misingi yao ni pamoja na kukanusha sifa za Allaah. Tunawaraddi kwa kuwaambia kwamba sifa si za mwingine isipokuwa yule mwenye kusifika kwazo, vivyo hivyo inapokuja kwa majina si ya mwengine isipokuwa yule mwenye kuitwa kwayo. Hivyo ni kosa kusema kwamba ni washirika wa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo wanawatuhumu wanaothibitisha sifa za Allaah kwamba ni washirikina. Haya yanajulisha ukafiri na upotevu wao. Mpaka ar-Raaziy wakati Ibn Khuzaymah alipotunga kitabu kinachozungumzia majina na sifa za Allaah kwa jina “Kitaab-ut-Tawhiyd” akakiita “Kitaab-ush-Shirki”[1]. Kwa sababu eti Ibn Khuzaymah anamthibitishia Allaah majina na sifa. Kwa mtazamo wake ar-Raaziy anaona kuwa Ibn Khuzaymah amemthibitishia Allaah washirika. Haya ndio madai yao. Wao wanapinga majina na sifa za Allaah eti kwa ajili ya Tawhiyd. Mpwekeshaji ni yule anayepinga majina na sifa za Allaah, ndivo wanavosema, na mshirikina ni yule anayethibitisha majina na sifa za Allaah. ´Aqiydah yao ni mbovu hata ikifanyiwa kazi kwa viumbe. Kwa mfano ukisema kuwa mtu fulani ni mwanachuoni, mtunzi na mkaguzi haina maana kwamba majina na sifa zake zimekuwa za viumbe wengine na washirika wake. Hakuna mtu mwenye akili anayesema hivo.

[1] at-Tafsiyr al-Kabiyr (27/170) ya ar-Raaziy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 29/07/2021