48. Du´aa wakati wa kuona matokeo ya kwanza


186- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

”Watu walipokuwa wakiona matokeo ya kwanza ya matunda wanakuja nayo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume anapoyachukua husema:

اللهُمَّ بارِكْ لَنَا في ثَمَرِنَا وَبَارِكْ لَنَا في مَدِينَتِنَا وَبَارِكْ لَنَا في صَاعِنَا وَبَارِكْ لَنَا في مُدِّنَا

”Ee Allaah! Tubarikie matunda yetu. Tubarikie mji wetu. Tubarikie Swaa´ yetu. Tubarikie Mudd yetu.”

Kisha humpa nalo mdogo katika watoto waliopo pale.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 21/03/2017