48. Dalili ya tano kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


46 – Nilimsomea Abul-´Abbaas Ahmad bin al-Mubaarak bin Sa´d bin al-Marqa´aatiy: Babu yenu Abul-Ma´aaliy Thaabit bin Bundaar bin Ibraahiym al-Baqqaal amekuhadithieni: Abu ´Aliy al-Hasan bin al-Husayn bin al-´Abbaas bin Duumaa ametuhadithia: Abu ´Aliy Makhlad bin Ja´far ametuhadithia: Abu Muhammad al-Hasan bin ´Aliy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Iysaa al-´Attwaar ametuhadithia: Abu Hudhayfah Ishaaq bin Bishr ametuhadithia, kutoka kwa Juwaybir, kutoka kwa adh-Dhwahhaak, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

“Mke wa azizi alisema kumwambia Yuusuf (´alayhis-Salaam): “Ee Yuusuf! Mimi nina lulu, mapambo na mawe ya thamani vingi. Niyatakupa yote ili umpe na umridhishe Mola wako aliye juu ya mbingu.”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Juwaybir ni Ibn Sa´d na ni mwenye kuachwa. Kuna maafikiano pia kwamba Ishaaq ni mwenye kuachwa. Ni mwenye kutuhumiwa uongo.” (al-´Uluww, uk. 88)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 143
  • Imechapishwa: 01/07/2018