Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye alama tatu ni mnafiki.”[1]

MAELEZO

Ni kwa nini mambo haya yameitwa kuwa ni unafiki? Kwa sababu yule ambaye anazungumza na nduguye anadai kuwa ni mkweli katika mazungumzo yake ilihali ukweli wa mambo anasema uongo. Anadhihirisha kitu ilihali anaficha kitu kingine. Anadhihirisha kitu kizuri na kuficha kitu kibaya.

Kadhalika inahusiana na mtu mwenye kufanya ahadi licha ya kuwa amenuia kuivunja. Anadhihirisha kitu kizuri na kuficha kitu kibaya.

Vivyo hivyo inahusiana na mtu mwenye kugombana na akaapiza katika magomvi yake. Anaonyesha uchaji na anaficha dhambi. Kadhalika anaapa hali ya kusema uongo, anashuhudia batili na akayaonelea halali yale aliyoharamisha Allaah ili aweze kushinda. Kwa sababu hii ndio maana haya yakaitwa kuwa ni unafiki, kwa sababu mwenye nayo anaonyesha kitu kizuri na anaficha kitu kibaya.

[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (59). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Alama za mnafiki ni tatu; anapoongea anasema uongo, anapoahidi anakhalifu na anapoaminiwa anafanya khiyana.”

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 162
  • Imechapishwa: 06/06/2019