47. Viongozi wanaowapendelea watu wao wa karibu na kuwaacha wananchi wakiwa masikini

Zayd bin Wahb ameeleza kupitia kwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baada yangu kutakuwepo mapendeleo na mambo msiyoyatambua.”

Mapendeleo. Viongozi watawapendelea wasapoti wao, watu wao wa karibu na ndugu zao kwa kuwapa nafasi na pesa. Watu watabaki wakiishi mafakiri. Wafanye nini? Hii ni dhuluma. Huku ni kuhukumu kwa wazi kinyume na yale aliyoteremsha Allaah. Allaah amesema juu ya hilo:

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesemaje juu ya hilo? Je, hivi nyinyi ni wajuzi zaidi wa Kitabu cha Allaah na dini Yake kuliko Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah watukufu na maimamu wote wa kale? Wakasema:

“Ee Mtume wa Allaah! Unatuamrisha nini yakimfika mmoja wetu hayo?” Akasema: “Watimizieni haki zilizo juu yenu na mumuombe Allaah haki zenu.”[2]

Usende katika mapambano. Usiandamane. Je, katika Uislamu kuna maandamano? Maji yakiisha kwa siku moja, wanatoka nje na kuandamana. Leo miji inatoa pasi na kuchukua. Leo miji mingi inawapa wananchi wao na hawachukui kutoka kwao isipokuwa kitu kidogo sana.  Ama kuhusu hawa walioko katika Hadiyth wanachukua, wanapendelea kwa pesa, hawatoi kitu na wanasababisha umasikini. Lau (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angeliamrisha kufanya uasi, basi Ummah ungeangamia. Badala yake akawaamrisha kuwa na busara, upole, subira na kuwa makini kwa ajili ya kuulinda Uislamu, kuisalimisha damu ya waislamu na kuichunga heshima yao:

“Watimizieni haki zilizo juu yenu na mumuombe Allaah haki zenu.”

[1] 05:44

[2] al-Bukhaariy (3603) na Muslim (1843).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 418-419
  • Imechapishwa: 23/10/2017