47. Swalah ya ijuma kwa wafanyakazi wanaoishi katika mji kwa muda fulani

Swali 47: Sisi ni kikosi cha wanajeshi na raia kutoka katika wafanyakazi wa ulinzi wa raia ambao tumekuja katika mji wa Riyaadh na maeneo mengine kwa ajili ya kuwahudumia wageni wa Mwingi wa rehema katika mwezi wa Dhul-Qa´dah na Dhul-Hijjah peke yake na tuko na msikiti ambao huswali ndani yake katika kipindi cha muda huu wa kazi. Je, inafaa kwetu kuswali ndani ya msikiti huu swalah ya ijumaa au tuswali Dhuhr[1]?

Jibu: Ni lazima kwenu kuswali pamoja na wengine ndani ya misikiti mikubwa ambayo wanaswali swalah ya ijumaa ikiwepesika kufanya hivo. Msipoweza basi swalini Dhuhr na wala msiswali ijumaa kwa sababu  nyinyi sio wakazi. Kwa sababu miongoni mwa sharti za kusihi swalah ya ijumaa ni wale watekelezaji wawe wakazi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/379-380).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 97
  • Imechapishwa: 05/12/2021