Swali 47: Ni vipi mwenye hedhi ataswali Rak´ah mbili za kuingia msikiti Mtakatifu? Je, inafaa kwa mwanamke mwenye hedhi kurudiarudia Dhikr kwa siri ndani ya nafsi yake?

Jibu: Mosi ni kwamba tunatakiwa kutambua hakuna swalah katika Ihraam. Haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliwasunishia Ummah wake swalah kwa ajili ya Ihraam; hakufanya hivo si kwa maneno wala vitendo vyake.

Pili ni kwamba mwanamke huyu mwenye hedhi ambaye amepata hedhi kabla ya kuhirimia anaweza kufanya Ihraam ilihali ni mwenye hedhi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Asmaa´ bint ´Umays, mke wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhumaa), wakati alipopata damu ya uzazi Dhul-Hulayfah akamwamrisha aoge, ajifunike kwa nguo na ahirimie. Vivyo hivyo mwenye hedhi pia ambapo anatakiwa kubaki kwenye Ihraam yake mpaka pale atapotwahirika. Kisha baada ya hapo atafanya Twawaaf katika Ka´bah na atafanya Say´.

Kuhusu kuuliza kwake kama inafaa kwake kusoma Qur-aan, ni uzuri ulioje kwa mwenye hedhi anayo haki ya kusoma Qur-aan wakati wa haja au wakati kuna manufaa fulani. Lakini bora ni yeye kutosoma ikiwa ni pasi na haja wala hakuna manufaa yanayopelekea yeye kufanya hivo isipokuwa tu anachotaka ni yeye kusoma kwa ajili ya kumwabudu Allaah na kujikurubisha kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 29/08/2021