47. Dalili ya nne kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


45 – Ahmad bin al-Mubaarak ametukhabarisha: Babu yangu upande wa mama Thaabit ametuhadithia: Abu ´Aliy bin Duumaa ametuhadithia: Makhlad ametuhadithia: al-Hasan bin ´Uluuyah ametuhadithia: Ismaa´iyl ametuhadithia: Ishaaq ametuhadithia: Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa al-Hasan ambaye amesema:

“Yuunus (´alayhis-Salaam) alisikia mawe na samaki wakisabihi ambapo na yeye mwenyewe akaanza kusabihi. Alikuwa akisema katika du´aa yake: “Mola wangu juu ya mbingu ndiko unakoishi na ardhini ndiko ulipo uwezo Wako na maajabu Yako. Mola wangu! Umenishusha chini kwenye mlima, ukanisahilishia kutembea ardhini na ukanizuia katika viza vitatu. Mungu wangu! Ulinifunga kwa gereza ambayo hukuwahi kumtia yeyote kabla yangu. Mungu wangu! Uliniadhibu kwa adhabu ambayo hukuwahi kumtia yeyote kabla yangu.” Zilipotimia siku arobaini na akapatwa huzuni akaita gizani: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe! Kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako! Hakika kweli nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Ishaaq bin Bishr alikuwa ni dhaifu na mwenye kuharibika.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (9/478))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 142-143
  • Imechapishwa: 21/06/2018