46. Uzinduzi na kuwatanguliza wanyonge kutoka Muzdalifah kwenda Minaa

Lau mwanamke atatufu na baada ya kumaliza Twawaaf akapatwa na hedhi katika hali kama hii atafanya Sa´y. Kwa sababu Sa´y haimshurutishii twahara. Mtunzi wa “al-Mughniy” amesema:

“Wanachuoni wengi wanaona kuwa kufanya Sa´y kati ya Swafaa na Marwah hakushurutishi twahara. Miongoni mwa wenye kuona hivo ni ´Atwaa´, Maalik, ash-Shaafi´iy, Abu Thawr na watu wa rai.” Mpaka aliposema: “Abu Daawuud amesema: “Nimemsikia Ahmad akisema: “Mwanamke akifanya Twawaaf kwenye Ka´bah kisha akapatwa na hedhi atafanya Sa´y baina ya Swafaa na Marwah kisha ataondoka zake. Imepokelewa kutoka kwa ´Aaishah na Umm Salamah kwamba wamesema: “Mwanamke akishatufu na akaswali zile Rak´ah za Twawaaf kisha akapatwa na hedhi, atembee kati ya Swafaa na Marwah.”[1]

12 – Inajuzu kwa wanawake kuondoka pale Muzdalifah na wale watu wanyonge baada ya mwezi kuzama na kupiga kile kiguzo cha ´Aqabah pindi watapofika Minaa kwa kuchelea msongamano wa watu. al-Muwaffaq amesema katika “al-Mughniy”:

“Hakuna neno kuwatanguliza wale wanawake wanyonge. Katika watu waliokuwa wakiwatanguliza watu wanyonge ni ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na ´Aaishah. Hayo pia ndio maoni ya ´Atwaa´, ath-Thawriy, ash-Shaafi´iy, na watu wa rai. Hatujui mwenye kusema kinyume. Pia katika kufanya hivo kuna kuwafanyia upole wale wanawake wanyonge, kuwaepusha na uzito wa msongamano na pia kuigiza kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

Imaam ash-Shawkaaniy amesema katika “Nayl-ul-Awtwaar”:

“Dalili zimefahamisha kwamba wakati wa kurusha vijiwe ni baada ya kuzama kwa jua kwa yule ambaye hana ruhusa. Wale wenye ruhusa kama vile wanawake na wanyonge wengine inafaa wakarusha kabla ya hapo.”[3]

Imaam an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´”:

“ash-Shaafi´iy na wenzi wao wamesema: “Sunnah ni kuwatanguliza wanyonge katika wanawake na wengineo kutoka hapo Muzdalifah kabla ya kuchomoza kwa alfajiri baada ya nusu ya usiku kwenda Minaa kupiga kile kiguzo cha ´Aaqabah kabla ya kusongamana kwa watu. Kisha akataja Hadiyth zinazofahamisha hilo.”[4]

[1] (05/246).

[2] (05/286).

[3] (05/80).

[4] (08/125).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 93-94
  • Imechapishwa: 14/11/2019