Uombezi ni haki. Lakini hata hivyo haiombwi kutoka kwa watu. Isipokuwa inaombwa kutoka kwa Allaah pekee. Kwa mfano unaweza kusema: “Ee Allaah! Nakuomba unipe uombezi wa Mtume  Wako”, “Ee Allaah! Nakuomba unipe uombezi wa waja Wako wema”. Usisimame mbele ya kaburi na kusema: “Ewe fulani… “, “Ewe Mtume wa Allaah… “ naomba uombezi. Kwa sababu maiti haombwi kitu. Bali uombezi unaombwa kutoka kwa Allaah pekee. Uombezi ni milki ya Allaah na sio milki ya mwingine yeyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 02/09/2018