Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Amelingana juu ya ´Arshi na ufalme Wake umezunguka.

MAELEZO

Kulingana juu ya ´Arshi kumetajwa sehemu saba ndani ya Qur-aan, ikiwa ni pamoja na “al-A´raaf”.

Ufalme ni Wake pekee. Amesema (Ta´ala):

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Amebarikika ambaye mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila jambo ni muweza.”[1]

فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

”Utakasifu ni wa ambaye mkononi Mwake kuna ufalme wa kila jambo na Kwake mtarejeshwa.”[2]

Ufalme wote ni wa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Viumbe wanaweza kumiliki kitu kidogo kisha baadaye kikawandoka. Amesema (Ta´ala):

تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Unampa ufalme Umtakaye na unamwondoshea ufalme umtakaye na unamtukuza umtakaye na unamdhalilisha umtakaye, kheri imo mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila jambo ni muweza.”[3]

Wafalme wa duniani wanao ufalme kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye kawamilikisha. Kisha baadaye anawaondolea ufalme ima kwa kufariki au kwa kupokonywa. Allaah pekee ndiye mwenye ufalme wa moja kwa moja na usiyokuwa na mpaka. Ufalme Wake hauondoki wala kumalizika.

[1] 67:1

[2] 36:83

[3] 3:26

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 31/07/2021