46. Tufanye nini na swawm ya msichana wetu?

Swali 46: Nina msichana wangu aliyefariki mwezi uliyopita. Ana siku sita zinazomlazimu za Ramadhaan. Ni lipi linalotulazimu juu ya swawm hiyo? Je, tumfungie, tumtolee swadaqah au hakuna linalotulazimu[1]?

Jibu: Ikiwa msichana wenu alikuwa anaweza kulipa lakini hamkulipa, basi hapo mtakuwa na wajibu wa kumfungia au kumlishizia kwa kila siku moja ambayo hakufunga. Ikiwa mtachagua hilo la pili mtatoa 1 kg mchele au ngano. Ama ikiwa maradhi yake yaliendelea mpaka akafariki si nyinyi wala yeye haimlazimu kitu.

[1] Kutoka ”Fath-ur-Rabb al-Waduud” (1/252).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 64
  • Imechapishwa: 13/06/2017