Swali 46: Ni ipi hukumu kwa mfungaji kutumia Siwaak baada ya jua kukengeuka?

Jibu: Mfungaji kutumia Siwaak kabla na baada ya jua kukengeuka ni Sunnah kama zilivyo Sunnah zengine. Kwa kuwa Hadiyth ni yenye kuenea katika utumiaji wa Siwaak. Hakuvuliwa mfungaji kabla wala baada ya jua kukengeuka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siwaak ni yenye kuusafisha mdomo na inamridhisha Mola.”[1]

“Lau nisingeliona uzito kwa Ummah basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”[2]

[1] Ahmad (47/06-62-124) na an-Nasaa´iy (05). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] al-Bukhaariy (887) na Muslim (510).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 39
  • Imechapishwa: 01/05/2021