Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ndio maana ya “hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”.

Katika Hadiyth:

“Kichwa cha mambo ni Uislamu, nguzo yake ni swalah na Jihaad katika njia ya Allaah ndio nundu yake ya juu.”[1]

Allaah ndiye Anajua zaidi. Swalah na salaam ziwe juu ya Muhammad, familia yake na Maswahabah zake.

MAELEZO

Ni juu ya kila yule ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia kumuabudu Allaah pekee pasi na vyengine vyote na kukufuru Twaaghuut na kuabudiwa kwake. Wanatakiwa washikamane na kumpwekesha Allaah, kufuata Shari´ah Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) na kuyaadhimisha maamrisho na makatazo Yake.

Kichwa cha mambo ni Uislamu. Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah. Yule atakayeishi kwa mujibu wa shahaadah anaingia katika Uislamu.

Nguzo yake ni swalah ambayo ndio nguzo ya pili. Swalah ndio nguzo kubwa baada ya shahaadah mbili. Halafu kunafuata zakaah, swawm, hajj na maamrisho mengine ya Allaah.

Nundu yake ya juu ni Jihaad katika njia ya Allaah. Kwa sababu kwayo dini inalindwa na kuhifadhiwa. Kwayo wanalinganiwa watu katika dini ya Allaah na wanalazimishwa kuinyookea haki. Kwa njia hiyo ndio nundu yake na Allaah ndiye anajua zaidi.

[1] Ahmad (5/231-237), at-Tirmidhiy (5/13) na Ibn Maajah (2/1394).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 17/02/2017