46. Makundi yenye kuwatukana Maswahabah


Mapote matatu ndio yenye uadui kwa Maswahabah:

1- Raafidhwah.

2- Khawaarij.

3- Naaswibah.

Lakini hata hivyo wabaya zaidi ni Raafidhwah.

Kilichowapelekea Khawaarij kufanya hivi ni kuwa na ususuwavu na kupetuka mpaka katika dini. Hawa malengo yao haikuwa kuutukana Uislamu. Walifanya hivi kwa sababu ya kupetuka mpaka na ususuwavu katika dini. Lengo lao haikuwa kuitukana dini. Bali haya – kwa madai  yao – ni kwa sababu ya kuipenda kwao dini na kuipupia.

Kuhusu Nawaaswib kilichowapelekea kuwatukana baadhi ya Maswahabah ni kwa sababu ya jambo la kisiasa. Wanachotaka kwa kufanya hivo ni kutukana uongozi wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Sababu ilikuwa jambo la kisiasa tu na kwamba hastahiki uongozi. Malengo yao pia haikuwa kuitukana dini.

Ama kuhusu Raafidhwah – Allaah awakebehi – malengo yao ilikuwa kuitukana dini. Endapo watawasema vibaya na kuwatukana Maswahabah, basi kutakuwa hakukubaki baina yetu sisi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukati na kati wowote ilihali dini imetufikia kupitia njia ya Maswahabah ambao – kwa mtazamo wa Raafidhwah – maneno yao hayatumiwi kama hoja. Kwa hivyo huku ni kuitukana dini. Haya ndio malengo yao.