46. Majimaji machafu yanayotoka kabla na baada ya hedhi

Swali 46: Ni ipi hukumu ya majimaji ya uchafu yanayomtoka mwanamke kabla ya hedhi kwa muda wa siku moja, zaidi ya siku moja au chini ya hapo?

Jibu: Ikiwa ni vitangulizi vya hedhi basi hiyo ni hedhi. Hilo linajulikana kwa yale maumivu ambayo kikawaida humjia mwenye hedhi. Kuhusu maji ya uchafuchafu baada ya hedhi anatakiwa kusubiri mpaka yaondoke. Kwa sababu maji ya uchafuchafu yaliyoambatana na hedhi huzingatiwa ni hedhi. Hilo ni kutokana na maneno ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Usifanye haraka mpaka uone mtiririko mweupe.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 38
  • Imechapishwa: 28/08/2021