49. Du´aa ya kumuombea mgonjwa wakati wa kumtembelea

  Download

147-

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

“Hapana neno; [ugonjwa] ni kusafishwa [madhambi] – Allaah akitaka.”[1]

148-

أَسْـأَلُ اللهَ العَـظيـم، رَبَّ العَـرْشِ العَـظيـم أَنْ يَشْفِـيَك

“Namuomba Allaah mtukufu, Mola wa ‘Arshi tukufu, akuponyeshe.”

Mara 7[2].

[1] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (10/118).

[2] ”Hakuna mja yeyote muislamu atakayemtembelea mgonjwa ambaye muda wake wa kufa haujafika akasema mara saba… ” at-Tirmidhiy na Abu Daawuud. Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (02/210) na ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (05/180).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/04/2020