46. Du´aa wakati mnyama wa mpando anapojikwaa


184- Kuna mtu ameeleza:

”Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mnyama wake ulipojikwaa. Nikasema: ”Shaytwaan aangamie!” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Usiseme ”Shaytwaan aangamie!” Ukisema hivo hujiona mpaka anakuwa mkubwa kama nyumba na kusema: ”Ninaapa kwa nguvu zangu” Badala yake sema:

بسم الله

”Kwa jina la Allaah.”

Ukisema hivo huogopa mpaka hujiona mdogo kama nzi.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 21/03/2017