46. Dalili ya ishirini na mbili kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah


48- Hishaam bin Hakiym amesimulia kwamba kuna mtu alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Matendo yaanze kufanywa au mipango imekwishapangwa?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah alitoa kizazi cha Aadam kutoka mgongoni mwake na akawashuhudisha juu ya nafsi zao wenyewe. Kisha akawamimina kwenye viganja vya mikono Yake na akasema: “Hawa wataingia Peponi na hawa wataingia Motoni.”[1]

Ameipokea al-Bayhaqiy.

[1] al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (712).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 33
  • Imechapishwa: 10/07/2019