46. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na tano wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akiifasiri Aayah:

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

“Na mtajeni Allaah katika siku za kuhesabika; atakayeharakisha [kuondoka kwake] katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake na atakayechelewesha basi hakuna dhambi juu yake, kwa anayemcha [Allaah kwa yote]. – Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.”[1]

“Abu Hamzah ath-Thimaaliy ameeleza kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema kuhusu Kauli ya Allaah:

وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ

“… na atakayechelewesha basi hakuna dhambi juu yake, kwa anayemcha [Allaah kwa yote].”

“Ninaapa kwa Allaah kwamba ni nyinyi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna wataobaki kuwa imara katika ukhaliyfah wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) isipokuwa wamchao Allaah.”[2]

Iko wapi Hadiyth hii batili na maana yenye kuenea ya Aayah, hukumu za hajj na rehema na uwasaa wake? Ni kana kwamba Aayah nyingi za Qur-aan hazina malengo mengine isipokuwa kuhusu uongozi wa ´Aliy. Aayah nyingi za Qur-aan zimepotoshwa kwa ajili ya Raafidhwah kwa sababu wanadai kuwa wako pamoja na ´Aliy na si pamoja na Allaah, dini Yake na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lengo lao tu ni uongozi wa ´Aliy. Hata hivyo hawako kabisa pamoja na ´Aliy; na ´Aliy amejitenga mbali kabisa na wao.

[1] 02:203

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/100).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 79
  • Imechapishwa: 19/03/2017