45. Shaytwaan kujigeuza maumbile ya wafu kwa lengo la kutaka kuwapotosha

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema ya kwamba mashaytwaan wanaweza kujigeuza umbile ya wafu. Halafu wakajitokeza kwa watu kwenye makaburi na wakasema “mimi ndiye fulani mwenye kaburi hili. Unataka nini?” Uhalisia wa mambo ni shaytwaan ambaye kajigeuza maumbile ya yule maiti. Matokeo yake watu wakadhani kuwa huyu ndio yule maiti. Shaykh amesema maneno yenye maana kama hiyo.

Vilevile anaweza kutoa mkono wake – kama walivosema – kwamba eti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoa mkono wake kumpa ar-Rifaa´iy wakasalimiana.” Huu ni uongo. Na ikiwa yametokea kweli, basi huyo ni shaytwaan. Mashaytwaan wanajigeuza kwenye makaburi kwa maumbile na sura za watu waliyomo ndani ya makaburi na wanasema au wao hawawaoni lakini wakaongea na wakadhani kuwa huyu maiti huyu ndiye anaongea ambapo wakasikia sauti zao. Matokeo yake yule anayemsikia akadhani kuwa ni sauti ya maiti. Haya yametokea sana. Kumbe shaytwaan anachotaka ni kuwapoteza katika shirki pasi nao kujua. Matokeo yake wakaliomba kaburi na wakaliomba uombezi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 70
  • Imechapishwa: 02/09/2018