45. Namna ya kukabiliana na wasiwasi ndani ya swalah


´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia:

“Ee Mtume wa Allaah! Hakika shaytwaan anaingia kati yangu mimi na swalah na kisomo changu na kunitatiza na kunishawisha.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Huyo ni shaytwaan anayeitwa Khinzab. Ukimuhisi basi unatakiwa kumuomba Allaah kinga na uteme cheche za mate kidogo upande wa shotoni mwako.” Nikafanya hivo na Allaah akamuweka mbali na mimi.”[1]

[1] Muslim na Ahmad. an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hadiyth inathibitisha ya kwamba imependekezwa kumuomba Allaah ulinzi kutokamana na shaytwaan na kutema mara tatu cheche za mate kidogo upande wa kushoto wakati anaposhawishi.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 111
  • Imechapishwa: 17/02/2017