45. Maneno ya Mujaahid kuhusu mikono ya Allaah


47- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Abu Yahyaa ambaye ameeleza kwamba Mujaahid amesema:

وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Mbingu zitakunjwa mkononi mwake mwa kuume.”33

“Mikono yote miwili ya Mwingi wa huruma ni ya kuume.” Nikasema: “Watu watakuweko wapi siku hiyo?” Akasema: “Juu ya daraja la Moto.”[1]

Imepokelewa na Israa’iyl kutoka kwa Abu Yahya.

[1] 39:67 ar-Radd ´alaa Bishr al-Mariysiy, uk. 36, na al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat” (709).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 33
  • Imechapishwa: 10/07/2019