45. Maisha ya wanandoa yanakuwa kutokamana na desturi


Nitamalizia maneno yangu kwa kidhibiti ambacho ni cha jumla juu ya haki za mume na mke. Kukaa kwao kunatakiwa kuwa kutokamana na ada na desturi ya watu. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na kaeni nao kwa wema.”[1]

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

Na hao wanawake wana kama ile [haki juu ya mume] iliyo juu yao kwa wema.”[2]

Wanachuoni wanasema kuwa Aayah ina maana ya kwamba waishi kutokamana na ada na desturi. Namna hii ndivyo wanandoa wanatakiwa kuishi. Katika hayo ni pamoja na wanandoa kushauriana, kila mmoja kuheshimu maoni ya mwingine na kusaidizana katika kila kinacholeta furaha. Mke amtake ushauri mume juu ya mambo yake, achukue maoni yake na amuheshimu na aiheshimu familia yake. Mume amtake ushauri mke wake, achukue maoni yake endapo ni ya sawa na aitendee wema familia yake. Mwanamke aone kwake wema mtupu kutokana na desturi ilivo.

[1] 04:19

[2] 2:228

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 24/03/2017