45. Hekima ya kwanza ya swawm: Kumwabudu Allaah

Yakishabainika hayo basi itambulike kuwa swawm ina hekima nyingi ambapo ikastahiki kuwa ni faradhi moja wapo miongoni mwa faradhi na nguzo moja wapo ya Uislamu.

Miongoni mwa hekima ya swawm ni kwamba ni kumwabudu Allaah (Ta´ala) ambapo mja anajikurubisha kwa Mola Wake kwa kujiepusha na vile anavyopenda na kutamani kama mfano wa vyakula, vinywaji na jimaa. Hivyo kunapata kudhihiri ukweli wa imani yake, ukamilifu wa kumwabudu Kwake Allaah, nguvu ya kumpenda Kwake Allaah na kutaraji yale yaliyoko Kwake. Hakika mtu haachi yale anayoyapenda isipokuwa kwa kitu ambacho kwake ni kitukufu zaidi.

Wakati ambapo muumini alijua namna ambavo Allaah anaifurahikia swawm kwa yeye kujiepusha na matamanio yake, ambayo kimaumbile ni mwenye kuyapenda, ndipo akatangulzia radhi za Mola Wake mbele ya matamanio yake. Hivyo kuyaacha ni matumaini makubwa kabisa anayokuwa nayo kwa Allaah. Kwani utamu wake na raha ya nafsi yake katika kuyaacha hayo amefanya kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo ndio maana utaona waumini wengi wanapopigwa au kutiwa jela ili waweze kufungua siku moja ya Ramadhaan bila udhuru wowote hawafungui. Hii ni miongoni mwa hekima tukufu na kubwa zaidi ya funga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 13/05/2020