45. Dalili ya pili kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


43- Katika ”Kitaab-ul-´Uruus” imekuja: Ahmad amesema: Muhammad bin Sa´d bin al-Husayn ametuhadithia: Ahmad bin Ibraahiym al-Mawsuliy ametuhadithia: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Hafws bin ´Abdillaah, kutoka kwa Hafsw bin ´Atwaa’ al-Khuraasaaniy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Sufyaan al-Alhaaniy, kutoka kwa Tamiym ad-Daariy ambaye amesema:

“Tulimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mtu kukumbatiana na nduguye pindi wanapokutana.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mtu wa kwanza aliyekumbatia alikuwa kipenzi wa hali ya juu wa Allaah ambaye ni Ibraahiym. Hilo lililkuwa siku moja wakati alipokuwa anachunga wanyama wake katika mlima mmoja wa Yerusalemu ambapo akasikia sauti akimtakasa Allaah. Akasahau kile kilichokuwa kinamshughulisha na akaanza kufuatilia ile sauti. Ghafla akamwona mtu mwenye nywele. Urefu wake ilikuwa dhiraa thamanini akimtakasa Allaah. Ibraahiym akamwambia: “Ee mzee! Ni nani Mola wako?” Akasema: “Ambaye yuko juu mbinguni.” Akamwambia: “Ni nani Mola wa Yule ambaye yuko mbinguni?” Akasema: “Ambaye yuko mbinguni.”Akamwambia: “Hakuna mungu wa haki mwingine mbinguni na ardhini isipokuwa Yeye?” Akaseam: “Hakuna mungu wa haki mwingine isipokuwa Yeye, Mola wa wale walioko mbinguni na Mola wa wale walioko ardhini.”Akamwambia: “Ee mzee! Je, uko pamoja na watu wako wengine?” Akasema: “Sijui kama kuna mwingine katika watu wangu aliye baki zaidi yangu.” Akamwambia: “Ni ipi lishe yako?” Akasema: “Hukusanya matunda ya mti huu wakati wa majira ya joto na huyala wakati wa majira ya baridi.” Akamwambia: ”Ni kipi Qiblah chako?” Akamuashiria Qiblah cha Ibraahiym (´alayhis-Salaam). Akamwambia: ”Nyumba yako iko wapi?”Akasema: ”Katika pango lile.”Akamwambia: ”Nenda nyumbani kwako.” Akasema: ”Kati yangu mimi na nyumba yangu kuna bonde lisilovukwa.”Akamwambia: ”Wewe huvuka vipi?” Akasema: ”Mkuja na mkwenda huvuka juu ya maji.”Ibraahiym akasema: “ Twende! Huenda Yule aliyekudhalilishia wewe atanidhalilishia na mimi.”Wakaanza mwendo. Baada ya muda wakayafikia maji waliyotembea juu yake. Kila mmoja akashangazwa na jambo la mwenzake. Wakaingia pangoni. Ibraahiym akatazam na kuona kuwa Qiblah chake yeye ndio Qiblah chake pia ambapo akamwambia: ”Ee mzee! Ni siku gani ambayo ni kuu?” Akasema: ”Ni ile siku ambayo Allaah ataweka Kursiy Yake kwa ajili ya hesabu. Siku hiyo Jahannam itaamrishwa kupumua na hakutobaki Malaika yeyote aliye karibu wala Mtume yeyote aliyetumwa isipokuwa ataenda chini asujudu. Kutokana na hali za Siku hiyo kila nafsi ni yenye kujiangalia.” Ibraahiym akamwambia: ”Ee mzee! Muombe Allaah anisalimishe mimi na wewe kutokana na hali za Siku hiyo.” Akasema: ”Nifanye nini na du´aa yangu? Mimi nina du´aa iliyozuwiliwa huko mbinguni. Sijaiona sasa miaka tatu.” Ibraahiym akamwambia: ”Nisikweleze kitu kinachoizuia du´aa yako?” Akasema: ”Ndio.”Akamwambia: ”Allaah (´Azza wa Jall) anapompenda mja, basi huchelewesha maombi yake kwa sababu ya kupenda sauti yake. Na anapomchukia mja, basi huharakisha maombi yake au humtia kukata tamaa kifuani mwake. Ni yepi maombi yako yaliyozuiliwa mbinguni kwa miaka tatu?” Akasema: “ Siku moja mahala papa hapa nilimpita kijana ambaye alikuwa na nywele zilizosukwa. Alikuwa na kondoo kana kwamba zilikuwa zimefungwa na ng´ombe kana kwamba zilikuwa na mafuta. Nikasema: ”Ninaapa kwa Allaah! Ni wa nani hawa?” Akasema: ”Ibraahiym (´alayhis-Salaam), kipenzi wa hali ya juu wa Allaah.” Ndipo  nikasema: “Ee Allaah! Kama kweli uko na kipenzi wa hali ya juu basi nionyeshe naye kabla ya mimi kutoka katika dunia hii.” Ibraahiym akasema: “Basi du´aa yako imeitikiwa.” Wakakumbatiana. Kabla ya hapo walikuwa watu wakisujudiana. Baadaye Uislamu ukaja na jambo la kupeana mikono. Vidole haviacheni mpaka kila mmoja anasamehewa. Himdi zote ni za Allaah ambaye ametuondoshea mizigo yao.”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Hadiyth ni batili na ndefu.” (al-´Uluww, uk. 556)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 140-141
  • Imechapishwa: 21/06/2018