45. Dalili juu ya vidole vya Allaah 4

45- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: al-´Abbaas bin al-Waliyd bin Yaziyd ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Ibn Jaabir ametuhadithia… al-Husayn bin Ismaa´iyl vilevile ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Yuunus as-Sarraaj ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Jaabir, kutoka kwa Busr bin ´Ubaydillaah al-Hadhwramiy, kutoka kwa Abu Idriys al-Kawhlaaniy: Nimemsikia an-Nawwaas bin Sam´aan al-Kullaabiy akisema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna moyo isipokuwa uko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mola wa walimwengu. Akitaka kuunyoosha, basi Anaunyoosha, na akitaka kuupotoa, basi Anaupotoa.”

Amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثبتنا عَلَى دِينِكَ

“Ee Mwenye kuzigeuza nyoyo. Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako. Mizani iko mkononi mwa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall). Anaishusha na anaipandisha.”

al-´Abbaas amesema:

“… iko kwenye vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall). Akitaka kuunyoosha, basi Anaunyoosha, na akitaka kuupotoa, basi Anaupotoa.”

Amesema vilevile:

ثبت قلوبنا عَلَى دِينِكَ

“Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako. Mizani iko mkononi mwa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall). Kuna watu Anawashusha na kuna watu Anawanyanyua mpaka siku ya Qiyaamah.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 92-94
  • Imechapishwa: 01/04/2018