45. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na nne wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akiifasiri Aayah:

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ

“Na pambaneni nao mpaka kusiweko fitnah na dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee. Wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.”

“Ibraahiym amesema: Mmoja wao katika waliopokea kwao amenieleza: “Uadui wa Allaah hautompata yeyote isipokuwa wauaji wa kizazi cha al-Husayn.” Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/87).

Allaah ametakasika kusifikiwa na uadui na hafanyi dhulumu wala uadui wowote:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا

“Hakika Allaah hadhulumu uzito wa atomu. Na ikiwa ni [kitendo] kizuri hukizidisha na hutoa kutoka kwake ujira mkubwa.”[1]

Mola Wako hamdhulumu yeyote. Uadui ni mbaya zaidi kuliko dhuluma. Allaah awaue wale wasiomkadiria vile anavostahiki.

Isitoshe Aayah inahusiana na Jihaad ili neno la Allaah liweze kuwa juu na kutokomeza shirki. Baatwiniy huyu anajaribu kukengeusha maana hii kubwa na kuipeleka katika maana ya batili ili kuzima hamu ya wale wanaouchukia Uislamu, waislamu na khaswa Maswahabah. Watu hawa hawatambui na wala hawastahiki uadilifu, wema na wala hakuna yeyote atayebeba mzigo wa mwenzake.

[1] 04:40

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 78
  • Imechapishwa: 19/03/2017