44. Ni kiasi gani mzee anatakiwa kuwapa masikini?


Swali 44: Mzee asipoweza kufunga badala yake anawalishiza masikini chakula kama inavyojulikana. Chakula hichi kinatakiwa kupima kiwango gani?  Inafaa kuwalishiza chakula masikini kwa kuwapa chakula cha mchana na cha jioni?

Jibu: Chakula kinatakiwa kiwe Mudd. Mudd ni sawa na gramu 600. Kwa ajili hiyo tunawaambia watu katika nchi hii watoe 1 kg kwa kuzingatia ya kwamba watu katika nchi hii wako katika hali nzuri na himdi zote zinamstahikia Allaah. Vinginevyo ni kuwa kiwango cha wajibu ni chini ya 1 kg.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 62
  • Imechapishwa: 13/06/2017