Shaykh (Rahimahu Allaah):

“Atakayeweka baina yake yeye na Allaah wakatikati ambapo anawaomba… “

Akawaomba kwa mfano kwa kusema: “Ewe Ahmad al-Badawiy!”, “Ewe ´Abdul-Qaadir!”, “Ewe Husayn!”, “Ewe ´Aliy!”, “Ewe fulani!” niokoe, nisalimishe, niponye maradhi yangu, nirudishie kitu changu. Wanawaita kwa majina yao. Hii ndio shirki kubwa. Kwa sababu hii ni du´aa. Du´aa ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Du´aa ndio ´ibaadah.”[1]

Bi maana ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Akiomba badala ya Allaah, basi hii ndio aina kubwa ya shirki. Ni mamoja huyo aliyemuomba ni Malaika, Mtume, mja mwema, jini au mtu.

[1] Ameipokea Ahmad (18386), Abu Daawuud (1479), at-Tirmidhiy (3247) na Ibn Maajah (3828). at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 69-70
  • Imechapishwa: 02/09/2018