44. Mume mbaya ni sababu ya ugomvi na talaka

Mume mwema anakuwa namna hii. Ama mume asiyekuwa mwema, huomba haki zake pasina kutambua ni haki zepi alizo nazo mke wake. Anatangamana naye kwa ubaya na kutokuwa na makubaliano haraka. Pale tu ambapo mke wake anamuomba kitu ameshakuwa na jeuri na upinzani. Akikariri maombi yake ameshakunja paji la uso na kuugeuza. Akiropokwa ameshampiga na kumvunja. Akiingia nyumbani anavaa mavazi yasiyokuwa mazuri. Akitoka nyumbani anavaa vizuri, anajitia manukato, anatana nywele na kutengeneza ndevu zake. Nyumbani ni kama kazini kwake. Bila ya shaka mambo kama haya yanapelekea katika ugomvi, talaka na fujo.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 60
  • Imechapishwa: 24/03/2017