44. Maovu ya nne: Kupaka rangi kucha na kuzikuza kuwa refu

04- Kupaka rangi kucha na kuzikuza kuwa refu

Jambo la nne: Hii ni desturi nyingine mbaya inayofanywa na wanawake wengi wa Kiislamu kutoka kwa wanawake waovu wa Ulaya. Nayo si nyingine ni kupaka rangi nyekundu ya vanishi kucha zao na kuyaacha makucha yao kuwa marefu. Ni jambo ambalo wakati mwingine linafanywa pia na baadhi ya vijana. Huku sio kubadilisha maumbile ya Allaah pekee, jambo ambalo linapelekea katika kupatwa na laana Yake kama tulivyopata kujifunza punde kidogo, bali pia kuna kujifananisha na wanawake wa kikafiri jambo ambalo limekatazwa katika Hadiyth nyingi[1]. Miongoni mwazo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[2]

Jengine ni kwamba ni jambo linaenda kinyume na maumbile:

فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا

“Umbile la asili la kumpwekesha Allaah ambalo kawaumba watu kwalo.”[3]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fitwr[4] ni mambo matano; kutahiri, kunyoa nywele sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapa.”

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alyhi wa sallam) alituwekea muda wa kukata masharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kwapa na kunyoa nywele za sehemu za siri ya kwamba zisiachwe zaidi ya siku arubaini.”[5]

[1] Nimezitaja Hadiyth hizi kwa utafiti katika kitabu “Hijaab-ul-Mar-ah al-Muslimah”, uk. 53-81.  Yule mwenye kutaka arejee huko.

[2] Ameipokea Abu Daawuud, Ahmad na vilevile ´Abd bin Humayd katika “al-Muntakhab” (02/92), at-Twahaawiy katika “al-Mushkil” kwa mlolongo wa wapokezi ulio mzuri kama nilivyobainisha katika chanzo kilichotajwa, uk. 80-81.

[3] 30:30

[4] Bi maana Sunnah. Mienendo ya Mitume (´alayhimus-Salaam) ambao tumeamrishwa kuwafuata. Hivyo ndivyo imetajwa katika “an-Nihaayah”.

[5] Ameipokea Muslim (01/153), Abu ´Awaanah (01/190), Abu Daawuud (02/195), an-Nasaa´iy (01/07), at-Tirmidhiy (04/07), Ahmad (03/122), Ibn-ul-A´rabiy katika “al-Mu´jam” (01/41), Ibn ´Uday (02/201), Ibn ´Asaakir (01/142/08) na mapokezi mengine ni yao isipokuwa ule upokezi wa kwanza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 203-207
  • Imechapishwa: 29/04/2018