44. Dalili ya kwanza kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

42- Abul-Fath Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy´ ametukhabarisha: Hamad ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Abu ´Amr bin Hamdaan ametuhadithia: al-Hasan bin Sufyaan ametuhadithia: Muhammad bin Yaziyd ar-Rifaa´iy ametuhadithia: Ishaaq bin Sulaymaan ametuhadithia: Abu Ja´far ar-Raaziy ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim bin Bahdalah, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati Ibraahiym alipotupwa ndani ya moto alisema: “Ee Allaah! Hakika wewe upekee juu ya mbingu na mimi nipekee ninayekuabudu ardhini.”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Cheni ya wapokezi ni nzuri. Kuna watu wengi wameisimulia kutoka kwa Ishaaq.” (al-´Uluww, uk. 21)

adh-Dhahabiy amesema pia:

”Nzuri.” (Kitaab-ul-´Arsh (50))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 139
  • Imechapishwa: 21/06/2018