44. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na tatu wa al-Baqarah


al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akiifasiri Aayah:

كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ

“Mmeandikiwa [shariy’ah] kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa wema [namna inayoeleweka katika shariy’ah]. Haya ni wajibu kwa wenye kumcha Allaah.” (02:180)

“´Ammaar bin Marwaan ameeleza ya kwamba alimuuliza Abu ´Abdillaah kuhusiana na Aayah hii ambapo akajibu: “Ni haki ambayo Allaah Ameiwajibisha kwa watu kuitoa kutoka katika mali zao kumpa mtu ambaye anasimamia jambo hili.” Nikasema: “Je, kuna mpaka wowote?” Akasema: “Ndio.” Nikasema: “Ni ngapi?” Akasema: “Angalau sehemu moja ya sita [1/6] na wingi wake sehemu moja ya tatu [1/3].”[1]

Allaah Amemtakasa Abu ´Abdillaah na uongo huu. Mwanzoni Allaah Alisema wazazi na ndugu wapate sehemu ya wasia. Baada ya hapo Allaah akafuta Aayah hii kwa Aayah za mirathi. Mtawala hana sehemu yoyote ya wasia huu. Hili ni miongoni mwa porojo za viongozi wa Raafidhwah ambazo wamezusha ili waweza kula kwa kutumia jina la mtu huyu. Wamezusha haki (ikiwa ni pamoja na khumus) kwa kutumia jina lake ambayo wameiwajibishia nayo wafuasi wao wasiokuwa na akili, mafukara na wenye mioyo isiyofanya kazi kuitoa.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/76).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 19/03/2017