43. Upingaji wa al-Bayhaqiy juu ya ugusaji hauna hoja yoyote

44- Abu Bakr al-Bayhaqiy amesema:

“Ama maneno Yake:

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

“Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[1]

haijuzu kuifasiri kama ni viungo vya mwili. Kwa sababu (´Azza wa Jall) hasifiwi sehemu. Wala kufasiriwa kama nguvu, ufalme, neema na mafungamano. Kwa sababu vinginevyo kutakuwa hakuna tofauti kati ya Ibliys na Aadam ambapo fadhilah zake zitakuwa ni zenye kupotea. Kwa hivyo sifa mbili hizo zinaweza kufahamika pasi na ugusaji.”[2]

45- Shaykh wetu – Allaah awe radhi naye – amesema:

“Upingaji wa al-Bayhaqiy juu ya ugusaji hauna hoja yoyote. Mapokezi yanasema kinyume na maneno yake.”

[1] 38:75

[2] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/127).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 32
  • Imechapishwa: 09/07/2019