43. Mzee asiyeweza kufunga anatoa kafara vipi?


Swali 43: Kuna mtu ni mzee na hawezi kufunga. Je, alishe maskini mmoja kwa kila siku moja au alishe masikini sitini katika mwezi?

Jibu: Alishe masikini mmoja kwa kila siku moja.

Atatakiwa kulisha masikini sitini pindi ataposema kuwa mgongo wa mke wake kwake ni kama mgongo wa mama yake (Dhwihaar). Haihusiani na kulisha katika Ramadhaan.

Lililo salama zaidi ni yeye alishe masikini kumi kukipita siku kumi za Ramadhaan, halafu alishe masikini kumi wengine kukipita siku kumi za Ramadhaan kisha alishe masikini kumi wengine mwishoni mwa Ramadhaan.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 61
  • Imechapishwa: 13/06/2017