43. Mlangu kuhusu ambaye hakuridhika kuapiwa kwa Allaah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiape kwa baba zenu. Atakayeapa kwa Allaah basi na aseme ukweli. Yule mwenye kuapiwa kwa Allaah basi aridhie. Yule ambaye hakuridhia sio katika Allaah.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri.

MAELEZO

Mwandishi anakusudia kwa kichwa cha khabari hiki kubainisha uwajibu wa kuridhika kwa kiapo japokuwa mtu atakuwa ni mwenye kutilia mashaka ukweli wa yule mwenye kuapa au pengine hata akawa anajua kuwa anasema uongo au kwamba ni mwenye kutuhumiwa uongo. Pamoja na hivyo anatakiwa kuridhia hukumu ya Kishari´ah na kuridhika na hilo. Kwa sababu watu hawana ya kutazama isipokuwa yale ya dhahiri. Kadhalika hakimu hana jengine analoweza kufanya kunapokosekana ushahidi isipokuwa kusikiliza ule ushahidi wa mashahidi au kiapo cha mtuhumiwa.

 1- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiape kwa baba zenu. Atakayeapa kwa Allaah basi na aseme ukweli. Yule mwenye kuapiwa kwa Allaah basi aridhie. Yule ambaye hakuridhia sio katika Allaah.”

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuapa kwa baba, mama wala viumbe wengineo. Mwanzoni mwa Uislamu na wakati  walipohajiri kwa mara ya kwanza kwenda al-Madiynah walikuwa wakifanya hivo. Ndipo wakakatazwa kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Atakayeapa kwa Allaah basi na aseme ukweli.”

Ni wajibu kwa ambaye anaapa kwa Allaah aseme ukweli na asidanganye. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuapa kiapo ilihali ni mwongo basi atakutana na Allaah hali ya kuwa amemkasirikia.”[2]

Ni wajibu kutahadhari kuapa kwa Allaah hali ya kudanganya na khaswakhaswa katika magomvi na wakati inapohusiana na kupokonya haki ya muislamu. Kwa ajili hiyo imekuja katika Hadiyth nyingine:

“Yule mwenye kupokonya haki ya muislamu kwa kiapo chake basi amejiwajibishia kwa Allaah Moto na ameharamishiwa Moto.” Wakauliza: “Hata kama inahusiana na kitu kidogo?” Akajibu: “Hata kama inahusiana na kokwa ya tende.”[3]

Ameipokea Muslim.

Ni wajibu kwa mtu kuyaepuka yote hayo na asichukue haki ya nduguye muislamu isipokuwa kwa dalili za Kishari´ah au kwa mtazamo wa Kishari´ah. Mtu akimtaka kuapa basi atahadhari asisemi uongo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuapiwa kwa Allaah basi aridhie.”

Haya ndio makusudio. Anatakiwa kuridhia na kukinaika. Hana jengine la kufanya kwa sababu yeye ndiye ambaye kazembea kwa sababu hakushuhudisha, hakuandika na wala hakutoa hoja. Ailaumu nafsi yake mwenyewe na aridhie kiapo cha Kishari´ah. Allaah atampa haki yake siku ya Qiyaamah.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye hakuridhia sio katika Allaah.”

Haya ni matishio makali juu ya yule asiyeridhia na asiyekinaika na hukumu ya Allaah.

Faida:

Kafara kwa mwenye kuapa kwa kusema uongo atubie na arudishe haki kwa wenye nayo.

[1] Ibn Maajah (2101) na al-Bayhaqiy (20512). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Ibn Maajah” (1708).

[2] al-Bukhaariy (2357) na Muslim (138).

[3] Muslim (137).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 136-137
  • Imechapishwa: 02/11/2018