43. Maovu ya tatu: Kukata nyusi


3- Kukata nyusi

Jambo la tatu: Ni yale yanayofanywa na baadhi ya wanawake pindi wanapozichonga nyusi zao hadi zinaonekana kama upinde au mwezi mwembamba. Wanafanya hivo eti kwa madai ya kujipamba. Haya ni miongoni mwa yale mambo aliyoharamisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamlaani yule mwenye kufanya hivo pale aliposema:

“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kuchanja [kufanya tattoo] na mwenye mwanamke mwenye kuchanjwa, mwanamke mwenye kutoa nyusi na mwenye kutolewa nyusi, mmwanamke mwenye kuchonga meno na mwenye kuchongwa meno na mwenye kubadilisha maumbile ya Allaah kwa ajili ya kupata uzuri.”[1]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (10/306), Muslim (06/166-167), Abu Daawuud (02/191), at-Tirmidhiy (03/16). ad-Daarimiy ameisahihisha (02/279), Ahmad (4129), Ibn Battwah katika “al-Ibaanah” (02/136/01) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 201-203
  • Imechapishwa: 27/04/2018