43. Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua jina:

1- Katika kurasa zinazokuja mbele kuna orodha ya majina teuzi yanayoafikiana na Shari´ah na lugha. Ingawa ni machache kiidadi lakini ni yenye baraka.

2- Kwa sababu jina ni la kale haina maana kwamba ni lizuri kwa sababu hiyo. Kuna majina ambayo ni ya kale lakini hata hivyo sikuyataja kwa sababu maana yake si yenye kukubaliwa.

Kuna majina vilevile ambayo ni ya kushirikiana kati ya jinsia zote mbili sikuyataja isipokuwa tu Asmaa´.

3- Unapotaka kuchagua jina kwa ajili ya mwanao basi unatakiwa kufikiria kuwa linaendana na familia yako na chaguo lako. Kwa ajili hiyo nimeacha kutaja baadhi ya majina yanayojuzu kwa sababu hayaendani na waarabu na kisiwa cha kiarabu.

Natija ya majina yasiyofaa ni kuwa utaona wale waliopewa wanabadili majina yao pindi wanapokuwa wakubwa ili yaendane na majina ya watu wa mji au na kabila.

4- Pale ambapo utakuwa umeamua kwa mfano moja ya jina liliyomo katika orodha, basi hakikisha kulitumia kwa njia mbalimbali; unapomzungumzisha nalo, linakupa kun-ya/laqabu baada yake na linanasibisha jina hilo mwenyewe.

Kujitahidi majina yote ya mtoto kuwa katika sura kama hii, ni jambo lenye ladha nzuri na usahihi mzuri kabisa.

5- La mwisho na la kumalizia ni kwamba: hakikisha nyumbani kwako hakukosi majina haya matukufu, makubwa na yenye baraka kama ´Abdullaah, ´Abdur-Rahmaan, Muhammad, Ahmad, Ibraahiym, ´Aaishah, Faatwimah…

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 30
  • Imechapishwa: 18/03/2017