37- Sanda zikiwa chache na wafu wakawa wengi basi itafaa kuwavika sanda watu wengi ndani ya sanda moja na atangulizwe upande wa Qiblah yule ambaye ni mwingi wao zaidi wa Qur-aan. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia:

“Ilipokuwa siku ya Uhud Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia Hamzah bin ´Abdil-Muttwalib ilihali amenyofolewanyofolewa na amekatwakatwa viungo ambapo akasema: “Lau kama si kumfanya Swafiyyah [kupatwa na huzuni ndani ya nafsi yake] basi ningelimwacha [mpaka wanyama wakali na ndege wakamla] ili Allaah amfufue kutoka kwenye matumbo ya ndege na wanyama wa kali. Akamvika sanda katika shuka moja [na ilikuwa] anapofunikwa kichwa chake basi miguu yake hubaki wazi na anapofunikwa miguu yake basi kichwa chake hubaki wazi. Hivyo akamfunika kichwa chake na hakuswaliwa yeyote katika waliokuwa mashahidi isipokuwa yeye tu na akasema: “Mimi ni shahidi wenu hii leo. [Akasema: “Wafu wakawa wengi na nguo zikawa chache.” Akasema:] “Walikuwa wakikusanywa watatuwatatu na wawiliwawili ndani ya kaburi moja na pakiulizwa ni nani ambaye ni mwingi zaidi wa Qur-aan ambapo anatangulizwa kwenye mwanandani. Watu wawiliwawili na watatuwatatu walikuwa walivikwa sanda moja.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Maana ya Hadiyth ni kwamba alikuwa akiigawa shuka moja baina ya kundi la watu ambapo anamvika sanda kila mmoja kwa baadhi yake kutokana na dharurah hata kama haikusitiri zaidi ya baadhi ya mwili wake. Hayo yanafahamishwa na sehemu ya mwisho ya Hadiyth kwamba alikuwa akiuliza kuhusu mwingi wao zaidi wa Qur-aan ambapo anamtanguliza kwenye mwanandani. Kama wangelikuwa wote kwa pamoja wanawekwa ndani ya shuka moja basi angeliuliza mbora wao kabla ya kufanya hivo ili hilo lisije kupelekea juisanda na kuirudisha upya.”

Ameyataja katika “´Awn-ul-Ma´buud” (03/165). Tafsiri hii ndio ya sawa. Kuhusu maneno ya ambao wameifasiri kidhahiri ni kosa linalokwenda kinyume na mtiririko wa kisa hiki, kama alivyobainisha Ibn Taymiyyah. Waliokuwa mbali zaidi na usawa ni wale waliosema:

“Shuka moja maana yake ni kaburi moja. “

Kwa sababu haya yametajwa katika Hadiyth na hivyo hakuna maana ya kurudi kulitaja.

Ameipokea Abu Daawuud (02/59), at-Tirmdhiy (02/138-139) ambaye ameifanya kuwa nzuri na Ibn Sa´d (juzu 03, q 01, uk. 08), al-Haakim (01/365-366) na mtiririko ni wake. al-Bayhaqiy amepokea kutoka kwake (04/10-11), Ahmad (03/128) na ziada ni yake. al-Haakim amesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim” na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

Mambo yalivo ni kwamba ni nzuri peke yake, kama ilivyotangulia kwenye nambari tatu masuala ya 32 ukurasa wa 53.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 24/02/2020