43. Du´aa wakati wa khasira


Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah (useme: A’uwdhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym). Hakika Yeye Ndiye As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).” (Fuswswilat 41 : 36)

181- Sulaymaan bin Surad amesema:

“Nilikuwa nimekaa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati watu wawili waligombana. Mmoja wao uso wake ukageuka mwekundu na mishipa yake ikavimba. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Mimi najua neno ambalo lau atalisema ataondokewa na kile anachohisi. Lau atasema:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

“Najikinga kwa Allaah kutokana na Shaytwaan Aliyewekwa mbali na Rahmah za Allaah.”

ataondokewa na kile anachohisi.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 111
  • Imechapishwa: 21/03/2017