46. Du´aa pindi kunapotokea kitu kisichomfurahisha mtu au akashindwa kufanya jambo

144-

قَدَّرَ اللهُ وَما شـاءَ فَعَـلَ

“Allaah amekadiria na akitakacho hufanya.”[1]

[1] ”Muumini mwenye nguvu ni bora na mwenye kupendwa zaidi na Allaah kuliko muumini dhaifu – wote wana kheri. Pupia yale yanayokunufaisha na mtake msaada Allaah na usivunjika moyo. Ukipatwa na kitu usiseme ´lau ningefanya kadhaa ingelikuwa kadhaa na kadha`. Badala yake sema:

قَدَّرَ اللهُ وَما شـاءَ فَعَـلَ

“Allaah amekadiria na akitakacho hufanya.”

Kwani hakika neno ´lau´ linafungua matendo ya shaytwaan.” Muslim (04/2052).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/04/2020