43. Daraja ya Hadiyth za “Haqq-uz-Zawjan”


Hizi ni baadhi ya nasaha za Kishari´ah ili kuijenga familia na kutekeleza haki za ndoa. Lau mume na mke watazitendea kazi basi wote wataishi katika furaha kubwa.

Nimetaja tu baadhi katika haki za wanandoa. Sikutaja Hadiyth hata moja isipokuwa baada ya kuichunguza mnyororo wake na kurejea katika maneno ya wanachuoni juu yake. Kutokana na hilo nimefikia juu ya kwamba Hadiyth hiyo ni nzuri ya kutosha kwa kutumiwa kama hoja. Kama nilivyosema sikutaja Hadiyth hata moja isipokuwa angalau itakuwa ni nzuri. Hadiyth [tulizozitaja] zimethibitishwa na ni zinazostahiki, na himdi zote ni za Allaah, ili kuzitumia kama hoja na kuzitendea kazi. Kwani hakika ni maneno ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 56-60
  • Imechapishwa: 24/03/2017