43. Dalili ya arubaini kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


41- Ahmad bin al-Mubaarak ametukhabarisha: Babu yangu Thaabit ametuhadithia: Abu ´Aliy bin Duumaa ametuhadithia: Makhlad bin Ja´far ametuhadithia: al-Hasan bin ´Aliy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Iysaa ametuhadithia: Ishaaq bin Bishr ametuhadithia: Ibn Jurayj ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ na Muqaatil, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

“Jibriyl alisema: “Ee Muhammad! Vipi iwapo ungemuona Israafiyl na kichwa chake kikiwa chini ya ´Arshi na miguu yake ikiwa chini kwenye ardhi ya saba? ´Arshi inatulia juu ya mabega yake. Wakati mwingine analemewa kwa sababu ya kumwogopa Allaah mpaka anakuwa kama ndege mdogo wa kifalme mpaka kunakuwa hakuna chenye kuweza kubeba ´Arshi ya Mola wako isipokuwa utukufu Wake.”[1][2]

[1] az-Zuhd, uk. 74, ya Ibn-ul-Mubaarak.

[2] adh-Dhahabiy amesema:

”Ishaaq bin Bishr alikuwa ni dhaifu na mwenye kuharibika.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (9/478))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 20/06/2018