43. Dalili juu ya vidole vya Allaah 2


43- al-Husayn bin Muhammad bin Sa´iyd al-Mutabbaqiy ametuhadithia: Muhammad bin Mansuur at-Twuusiy ametuhadithia: Abu Ahmad az-Zubayriy ametuhadithia: Sufyaan amesema, kutoka kwa al-A´mash, kutoka Abu Sufyaan, kutoka kwa Jaabir aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema: “Ee Mwenye kuzigeuza nyoyo. Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako.” Baadhi ya Maswahabah wake wakasema: “Unachelea juu yetu ilihali tumekuamini na tumekuwa na yakini juu ya yale uliyokuja nayo kwetu?” Akasema: “Ni kipi kinachonijuza? Hakika nyoyo za viumbe ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Allaah (´Azza wa Jall).”

Abu Ahmad akatikisa kidole chake.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 90-92
  • Imechapishwa: 01/04/2018