43. Anataka Ibn Baaz amwombee du´aa kwenye kaburi la Mtume

Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa X – Allaah amuwafikishe. Aamiyn.

Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh

Baada ya hayo; barua yenu tukufu ya tarehe 03/03/1974 M imefika – Allaah akuunganishe kwa uongofu Wake – na yale imejumuisha yametambulika. Tunakupongeza kwa kuoa. Allaah ajaalie iwe ndoa iliyobarikiwa. Umetaja katika barua yako kwamba tukuombee du´aa kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Nakufahamisha kuwa kuomba du´aa karibu na kaburi ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Ni mamoja kaburi hilo ni la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au la mwengine. Isitoshe sio pahali pa kuitikiwa. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kulitembelea, kuwatolea salamu wale wafu, kuwaombea du´aa, kukumbuka Aakhirah na kifo. Nimependa kukuzindua juu ya hilo ili uwe juu ya utambuzi. Unaweza kurejelea Hadiyth zinazozungumzia matembezi mwishoni mwa chuo cha jeneza katika Buluugh-ul-Maraam ili utambue jambo hilo. Allaah atuwafikishe sisi na nyinyi kufuata Sunnah, kufanyia kazi yale yanayomridhisha Yeye (Subhaanah) na kukurubisha katika dini Yake.

wa as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 25/07/2022