43. al-Qummiy upotoshaji wa kumi wa al-Baqarah


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗكَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ

“Na watasema wale waliofuata: “Lau tungekuwa tunamiliki kurudi [duniani] tungewakana kama walivyotukana.” Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha ‘amali zao kuwa ni majuto juu yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.” (02:167)

“Mansuur bin Haazim amesema: “Nilimwambia Abu ´Abdillaah:

وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ

“Na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.”

Akasema: “Ni wale maadui wa ´Aliy ambao watakuwa ni wenye kudumishwa Motoni milele.”[1]

Anawakusudia Maswahabah watukufu na khaswa Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum). Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Raafidhwah ndio maadui wa ´Aliy kama jinsi manaswara ni maadui wa ´Iysaa. ´Aliy na ndugu zake walikuwa na mpanzi ya hali ya juu kati yao. Hawa Raafidhwah Baatwiniyyah ni maadui wa wote hao.

Kisha mtu anaweza akajiuliza ni kwa nini maadui wa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika makafiri na washirikina wasitishwe. Kwa vile wao ndio wenye kukusudiwa na Aayah hii. Lakini Raafidhwah hawajali haki za Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndio maana kila kitu wanakifungamanisha na ´Aliy na watu wa familia ya Mtume na wanafanya hivo kwa kutumia uongo. Watu wa familia ya kwa Mtume ni wenye kujitenga mbali kabisa na matendo haya. Wanajiona wao kama Waislamu kwa kiasi na wanatambua ni hadhi gani Maswahabah wako nayo ambapo wanawaadhimisha na khaswa Makhaliyfah watatu.

[1] Tafsiyr al-Qummiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 77
  • Imechapishwa: 19/03/2017