54. Mlango wa kutosema “Mja wangu, kijakazi wangu”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiseme mmoja wenu: “Mlishe mola wako,  mpe maji mola wako.” Bali badala yake aseme: “Bwana wangu, mlinzi/bosi wangu.” Wala asiseme mmoja wenu: “Mja wangu, mjakazi wangu.” Badala yake aseme: “Kijana changu, msichana wangu na mvulana wangu.”[1]

MAELEZO

Mlango huu unabainisha baadhi ya mambo yanayopingana na ukamilifu wa Tawhiyd. Wakati mtu anapomzungumzisha mvulana wake au mfanyakazi wake wa kike asiseme: “Mja wangu, kijakazi changu.” Huku ni kwa ajili ya kufanya adabu na Allaah (Ta´ala). Bali anatakiwa kusema kwa mfano: “Kijana changu, msichana wangu, mvulana wangu, mfanyakazi wangu”. Kwa sababu waja wote ni waja wa Allaah, wajakazi wote ni wajakazi wa Allaah. Haya ni kwa minajili ya ukamilifu wa Tawhiyd na kufanya adabu na Allaah (´Azza wa Jall) pamoja vilevile na kumtambua Allaah (Subhaanah) kwamba Yeye ndiye mfalme wa kila kitu na ndiye Mwenye kukiendesha kila kitu.

Hata hivyo mtu akisema mtumwa wa fulani au mjakazi wa fulani kwa njia ya kuelezea, ni jambo jepesi kidogo na si kwamba anajiegemezea kwake mwenyewe.

1- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiseme mmoja wenu: “Mlishe mola wako, mpe maji mola wako.” Bali badala yake aseme: “Bwana wangu, mlinzi/bosi wangu.” Wala asiseme mmoja wenu: “Mja wangu, mjakazi wangu.” Badala yake aseme: “Kijana changu, msichana wangu na mvulana wangu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiseme mmoja wenu: “Mlishe mola wako, mpe maji mola wako.”

Haya ni kwa minajili ya kufanya adabu. Kwani Mola wa wote ni Allaah. Allaah (Ta´ala) halishwi. Yeye hamuhitajii yeyote. Haitakikani kusema hivo kwa njia ya moja kwa moja. Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Bwana wangu, mlinzi/bosi wangu.”

Msemo mwingine ni ´ami´. Kwa sababu msemo huu ni wenye kutambulika na haupingani na uola wa Allaah. Bwana ni yule mmiliki na raisi. Yeye ndiye mmiliki wa kijana huyu. Vilevile bosi au mlinzi ni neno lenye maana nyingi ikiwa ni pamoja na mmiliki, mtu aliye karibu na msaidizi.

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Asiseme mmoja: “Mlinzi/bosi wangu.” Kwa sababu Mlinzi ni Allaah.”

Lakini kilichohifadhiwa kwa wanachuoni ni ule upokezi unaoruhusu kusema hivo. Neno ´mlinzi` wengine pia wanaweza kuitwa hivo. Allaah (Ta´ala) amesema:

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye Mlinzi wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.” (Muhammad 47:11)

Bi maana hawana mwenye kuwanusuru. Ni wenye kukoseshwa nusura inapokuja katika mlinzi juu ya hesabu ya Allaah. Kwa hiyo hakuna neno kutumia msemo wa ´bwana` na ´mlinzi/bosi`. Hii leo imekuwa ni jambo la kawaida watu kutumia msemo wa ´ami` na mfano wake badala ya ´mola`.

[1] al-Bukhaariy (2552) na Muslim (2249).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 155
  • Imechapishwa: 06/11/2018