42. Wafungwa kuswali mkusanyiko nyuma ya imamu mmoja kupitia kipaza sauti

Swali 42: Nimerejea barua yako nambari. 275 tarehe 1405-05-01 ambapo unauliza hukumu ya swalah ya ijumaa na ya mkusanyiko ya wafungwa nyuma ya imamu mmoja ambaye anawatangulia mbele ilihali wako katika wadi/vyumba vyao kupitia kipaza sauti[1].

Jibu: Kwa kuzingatia kwamba swali ni la muhimu na lenye kuenea nikaona niliwasilishe katika baraza la kikao cha Kibaar-ul-´Ulamaa´. Baraza wamelipitia katika kikao chake cha ishirini na sita kilichofanyika Twaaif tarehe 1405-10-25 mpaka 1405-11-07. Baada ya kusoma na kulikagua suala hilo kutokana na maono ya wanazuoni juu ya maudhui hayo. Wametoa fatwa juu kutofaa kuwakusanya wafungwa kwa imamu mmoja katika swalah za ijumaa na swalah za mkusanyiko wakiwa ndani ya wadi za gereza wakimfuata kupitia njia ya spika. Swalah ya ijumaa sio lazima kwao kwa sababu hawawezi kuiendea. Hilo ni pamoja na kwenda sambamba na fatwa ya Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) nambari. 762 tarehe 1388-10-11 aliposema kwamba si lazima kuitekeleza regezani na kutokana na sababu nyingine.

Lakini ambaye itamyumkinia kuhudhuria kutekeleza swalah ya ijumaa katika msikiti wa gereza – kukiwa kuna msikiti ambapo kunaswaliwa swalah ya ijumaa – basi ataiswali pamoja na wengine. Vinginevyo ni yenye kudondoka kutoka kwake na badala yake ataiswali Dhuhr. Kila mkusanyiko wa watu wataswali zile swalah tano mkusanyiko ndani ya mabweni yao ikiwa haitowezekana kuwakusanya ndani ya msikiti au sehemu moja.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/345-346).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 05/12/2021